Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila leo Oktoba 15, 2025 amekagua miradi ya ujenzi wa madaraja na barabara jijini Dar es Salaam inayojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 224.22.

Chalamila amebainisha kuwa kukamilika kwa miradi hiyo inayotekelezwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kutarahisisha huduma za wananchi na kuchochea maendeleo ya mkoa, ikiwa ni pamoja na kuepuka vifo visivyo vya lazima.

Amewataka wakandarasi wa miradi hiyo kuhakikisha wanakamilisha kazi hizo ndani ya muda uliopangwa.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *