Takriban watu 16 wamefariki dunia baada ya moto mkubwa kuzuka katika kiwanda cha nguo nchini Bangladesh, huku maafisa wakionya k...

Takriban watu 16 wamefariki dunia baada ya moto mkubwa kuzuka katika kiwanda cha nguo nchini Bangladesh, huku maafisa wakionya kuwa huenda idadi hiyo ikaongezeka.

Miili kumi na sita imepatikana lakini ilichomrka kiasi cha kutotambulika, shirika la zima moto limesema.

Jamaa waliofadhaika walikusanyika nje ya kiwanda cha ghorofa nne katika eneo la Mirpur huko Dhaka siku ya Jumanne kuwatafuta wapendwa wao ambao bado hawajapatikana.

Moto huo uliozuka katika kiwanda hicho mwendo wa saa sita mchana, ulizimwa baada ya saa tatu. Lakini ghala la kemikali lililo karibu liliendelea kuwaka, serikali ilisema.

Mkurugenzi wa huduma ya zima moto Mohammad Tajul Islam Chowdhury aliambia vyombo vya habari vya ndani kuwa waathiriwa walikufa “papo hapo” baada ya kuvuta “gesi yenye sumu kali”.

Polisi na maafisa wa kijeshi bado wanajaribu kuwatafuta wamiliki wa kiwanda na ghala hilo, Bw Chowdhury aliambia wanahabari.

Uchunguzi kuhusu iwapo ghala hilo lilikuwa likifanya kazi kihalali pia unaendelea, aliongeza.

Wanafamilia waliokuwa na machozi walisimama nje ya majengo yaliyokuwa yameungua, wengi wao wakiwa wameshikilia picha za jamaa zao waliopotea.

#chanzobbcswahili
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *