
Chanzo cha picha, Getty Images
Klabu ya Italia Inter Milan imeingia kwenye kinyang’anyiro cha kumsajili beki wa kati wa Crystal Palace Marc Guehi lakini Liverpool bado wanapewa nafasi kubwa ya kuinasa saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25. (Tuttosport – In Itali)
Mshambulizi wa Bournemouth Antoine Semenyo ana kipengele cha kuachiliwa huru katika kandarasi yake lakini Cherries wanaficha hilo kwa sababu wanataka kusalia na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana mwenye umri wa miaka 25 ambaye amekuwa akihusishwa na Tottenham na Manchester United. (Sportsport)
Chelsea na Barcelona wanamfuatilia mshambuliaji wa Dinamo Zagreb Mreno Cardoso Varela, 16. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images
Brighton hawana mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Cameroon Carlos Baleba mwezi Januari licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuvutiwa na Manchester United msimu uliopita. (Sportsport), nje
Manchester United wamemweka kiungo wa kati wa Crystal Palace na England Adam Wharton, 21, juu ya Baleba kwenye orodha ya wachezaji inaowalenga ili kuhamia timu hiyo. (Subscription Required)
Manchester United wanafikiria kuongeza mkataba wa kiungo wa kati wa Brazil Casemiro zaidi ya msimu huu, lakini tu ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 atakubali kupunguziwa mshahara. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kumekuwa na nia ya kumnunua Casemiro huko Brazil na Saudi Arabia lakini kocha wa Manchester United Ruben Amorim anaweza kuwasilisha hoja ya mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid asalie. (ESPN)
Mlinda lango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 33, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kuondoka katika klabu hiyo licha ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kuvutia vilabu vikiwemo Manchester United na Newcastle United. (Diario AS – In Spanish)
Beki wa Crystal Palace Daniel Munoz anasakwa na Barcelona lakini The Eagles hawatamruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye umri wa miaka 29 kuondoka mwezi Januari. (Fichajes – In Spanish),

Chanzo cha picha, Getty Images
Uamuzi wa aliyekuwa afisa mkuu wa kandanda wa Tottenham Scott Munn kuchukua nafasi katika klabu ya Parma ya Italia badala ya Nottingham Forest ni dalili zaidi kwamba kocha Ange Postecoglou yuko katika mazingira ya kupoteza kazi yake. (Sportsport)
Mkurugenzi mpya wa michezo wa Newcastle Ross Wilson ataongoza ukaguzi wa hali ya kandarasi ya wachezaji wakuu wa klabu hiyo huku klabu hiyo ikitarajia kumaliza marudio ya sakata ya uhamisho ambayo ilimfanya mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 26, kujiunga na Liverpool. (Subscription Required).

Chanzo cha picha, Getty Images
Chelsea hawana wasiwasi wowote kuhusu mustakabali wa kiungo wa Ecuador Moises Caicedo, 23, kufuatia ajenti wake kuadhibiwa hadharani. (Telegraph – Subscription Required)
Caicedo anatarajiwa kutuzwa kandarasi mpya na Chelsea ili kuzuia nia ya Real Madrid. (TeamTalks)
Borussia Dortmund wanavutiwa na kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Guille Fernandez mwenye umri wa miaka 17 ambaye bado hajacheza katika kikosi cha kwanza katika klabu hiyo ya Catalan. (Bild – In Deutch)