
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa leo mjini Gebneva na Port-au-Prince kiwango hiki ni cha juu kabisa kuwahi kurekodiwa nchini humo na ni ongezeko la asilimia 36 tangu mwishoni mwa mwaka 2024.
Grégoire Goodstein, Kiongozi wa IOM nchini Haiti amesema “Ukubwa wa mgogoro huu unahitaji msaada wa haraka na endelevu”.
Ameeleza kuwa jamii za ndani pamoja na washirika wa kimataifa lazima watoe msaada wa dharura kwa waliokumbwa kwa waathirika
Mgogoro unapanuka zaidi ya mji mkuu
Mikoa ya Centre na Artibonite Iko Hatua Mbaya
Kwa mujibu wa IOM ufurushwaji wa watu sasa unapanua wigo hauko tena kwenye mkusanyiko mkubwa tu wa mji mkuu Port-au-Prince.
Inasema karibu asilimia mbili ya tatu ya wau wapya walofurushwa wametokea nje ya mji mkuu, hasa katika mikoa ya Centre na Artibonite.
Ripoti zinaonesha mwenendo unaoendelea wa watu kuhamia maeneo ya miji kutokana na ghasia, jambo linaloweka shinikizo zaidi kwa jamii ambazo tayari zina rasilimali chache.
Jamii za ndani zinaubeba gharama kubwa ya ghasia
Shirika hilo la uhamiaji liinasema maeneo yaliyopo ya kuhamishia watu yamejaa na yakikosa huduma za msingi, huku idadi ya maeneo ya kuhamishia watu kwa hiari yakiongezeka kutoka 142 Desemba 2024 hadi 238 Oktoba 2025.
Karibu asilimia 85 ya watu waliofurushwa makwao wanapewa hifadhi na familia za wenyeji, jambo linaloonesha shinikizo kubwa kwenye rasilimali zilizopo. Wanawake na watoto ndio kundi linaloathirika zaidi, na familia nyingi zimegawanyika ili kutuma watoto katika maeneo salama imesema IOM.
Shinikizo katika mipaka ya nchi
Shirika la IOM limetanabaisha kwamba jamii zilizo kando ya mpaka wa Haiti na Jamhuri ya Dominika zinakabiliana na changamoto zaidi baada ya Waihati zaidi ya 207,000 kurudishwa tangu Januari 2025.
Watu hawa wanarudi kwenye nchi yenye ghasia za makundi ya uhalifu, jambo linaloongeza ugumu wa juhudi za kibinadamu na utoaji wa huduma muhimu.
Ombi la msaada kwa jumuiya ya kimataifa
Katika hatua za msada IOM imepanua shughuli zake nje ya Port-au-Prince, ikitoa makazi ya dharura, maji safi, huduma za afya, msaada wa afya ya akili na kisaikolojia, ulinzi, na fursa za maisha kwa familia zilizo hatarini.
Uhirikiano na mamlaka na wanajamii unalenga kuimarisha umnepo kupitia elimu, programu za vijana, na ukarabati wa miundombinu.
IOM inaisisitiza jumuiya ya kimataifa kuongeza ufadhili na upatikanaji wa msaada kuhakikisha misaada inafikishwa kwa wale walio hatarini zaidi huku ikichangia pia katika suluhisho za muda mrefu kupunguza watu kukimbia makwao.