ZILIZOBAMBA MITANDAONI: Mtangazaji wa soka @ngodaalwatan asimulia namna anavyomkumbuka Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amo...

ZILIZOBAMBA MITANDAONI: Mtangazaji wa soka @ngodaalwatan asimulia namna anavyomkumbuka Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Amolo Odinga ambaye amefariki dunia leo nchini India ambako alikuwa anapatiwa matibabu.

Wachambuzi @akingamkono na @sharif_bayona nao waeleza namna wanavyomkumbuka kwenye medani za siasa na soka pia.

Odinga alikuwa shabiki mkubwa wa Gor Mahia, timu ambayo alikuwa kama Rais wao, mdhamini na kila kwenye matukio makubwa ya timu hiyo, alihudhuria.

Inaelezwa kuwa mara nyingi ‘Kogalo’ walipokuwa na changamoto ya kifedha, Odinga aliweka mkono wake na alijiita kuwa ni shabiki nambari moja wa Gor Mahia.

#Viwanjani #Zilizobamba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *