Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema kuhusu taarifa ya mwisho ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) kwamba: “Kwa mtazamo wa jumuiya hiyo, Azimio nambari 2231 la Umoja wa Mataifa bado ni halali na vipenege na muda wa azimio hilo vinapaswa kuzingatiwa.

Sayyid Ababs Araqchi amesema katika mahojiano na shirika la habari la IRNA akiwa mjini Kampala kwamba: “Leo kumefanyika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumui ya Nchi Zisizofungamana na Siasa za Upande Wowote (NAM) huko Uganda. Jumuiya hiyo inashughulikia masuala yote ya kimataifa, masuala yote ya ustawi wa kiuchumi, kijamii na kisiasa.”

Ameongeza kuwa: Taarifa ya mwisho au hati  ya mwisho ya mkutano wa NAM mjini Kampala ina vipengee zaidi ya 1,500. Kuna vifungu viliongezwa kwa pendekezo lililotolewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ambapo muhimu zaidi ni kulaaniwa vikali mashambulizi ya utawala wa Kizayuni na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Aidha maneno kama mashambulizi ya kutisha na yasiyokubalika yametumika sambamba na neno la kudhihirisha mshikamano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. 

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran amesema kuwa: Tamko hili la kulaaniwa vikali mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limetolewa kwa nyakati tofauti katika taarifa ya Kampala na kujumuishwa pia katika hati ya mwisho ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya NAM sawa kabisa na ilivyoarifishwa katika kipengee maalumu suala la kulaaniwa mashambulizi dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.

Sayyid Abbas Araqchi pia amesitiza kuwa hata hivyo kuna kipengee kimoja ambacho kimejumuishwa katika mkutano huo na pia katika hati ya mwisho ambacho kina umuhimu mkubwa, nacho ni tangazo la kuungwa mkono Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuhusu suala la Snapback katika Baraza la Usalama na kuwekwa wazi kuwa, kwa mtazamo wa jumuiya ya NAM, azimio nambari 2231 bado ni halali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *