#HABARI: Mama mzazi wa aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole na baadhi ya ndugu wakiingia Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam kwa ajili ya muendelezo wa usikilizaji wa shauri la Polepole.

Mahakama hiyo imepanga hii leo Oktoba 16, 2025 kutoa uamuzi juu ya maombi ya Jamhuri ya kutaka kuwahoji maswali ya dodoso Wakili Peter Kibatala na Godfrey Polepole.

Hatua hiyo imekuja baada ya wakili wa wajibu maombi Faraji Nguka kuieleza Mahakama mbele ya Jaji Salma Maghimbi ya kwamba wanaomba kuwahoji Kibatala na Godfrey Polepole kutokana na mkanganyiko uliopo kwenye kiapo kinzani.

Maombi hayo yamepingwa na Wakili Kibatala akisema kuwa endapo Mahakama itaruhusu ombi hilo italazimika kutoa nafasi kwa pande zote.

Maombi ya msingi katika kesi hiyo yamefunguliwa na polepole kupitia Wakili Peter Kibatala aliyeiomba Mahakama itoe amri ya Polepole kufikishwa Mahakamani ama mamlaka ziseme alipo.

•Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *