#HABARI: Seif Msumari Hozza (26), Mkazi wa Luchelele na mfanyabiashara, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, kwa tuhuma za kulawiti mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 (jina limehifadhiwa kwa sababu za kisheria).

Akisoma hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mhe. Aman Sumari, Wakili wa Serikali Rose Kimaro ameieleza Mahakama kuwa tukio hilo lilitokea kati ya mwezi Agosti na Septemba 2025 katika eneo la Siluvin, Kata ya Luchelele jijini humo, ambapo mshtakiwa anadaiwa kutenda kitendo hicho cha ukatili dhidi ya mtoto huyo.

Katika kesi hiyo ya jinai yenye namba 25168/2025, mshtakiwa anakabiliwa na shtaka moja la kulawiti, kinyume na Kifungu cha 154(1)(a)(2) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marejeo ya mwaka 2023.

Hata hivyo, mshtakiwa amekana shtaka hilo, Hakimu Sumari anayesikiliza kesi hiyo ameeleza kuwa kosa hilo linadhaminika kwa masharti, ikiwemo kuwa na wadhamini wawili wenye vitambulisho halali vya taifa, barua za utambulisho kutoka serikali ya mtaa na kila mdhamini kusaini hati ya dhamana ya Shilingi milioni nne.

Mshtakiwa ameshindwa kukidhi masharti ya dhamana, hivyo amerejeshwa rumande hadi Oktoba 23, 2025, kesi hiyo itakapoitwa kwa ajili ya kusomewa hoja za awali na usikilizwaji.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *