#HABARI: Shahidi wa tatu katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu ambaye ni Mkaguzi wa Jeshi la Polisi kutoka Kitengo cha picha Kamisheni ya Uchunguzi wa Sayansi Jinai Makao Makuu Dar es Ealaam, Samweli Kaaya (39) ameieleza Mahakama alivyofanya uchunguzi wa picha mjongeo ili kubaini kama ulikuwa ni picha halisi au ya kutengenezwa.
Samweli ambaye ameanza kutoa ushahidi hii leo, baada ya shahidi namba mbili kuhitimisha kutoa ushahidi katika kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu ambayo ipo katika hatua usikilizwaji wa mashahidi wa Jamhuri.
Shahidi huyo ambaye ni wa tatu kwa upande wa Jamhuri, alieleza hayo katika Mahakama Kuu Masjala ndogo Dar es Salaam, mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, akisaidizana na Jaji James Karayemaha na Ferdinand Kiwonde.
Awali, kabla ya shahidi wa tatu kuanza kutoa ushahidi, Lissu alimalizia sehemu ya maswali yake ya dodoso kwa shahidi wa pili ambaye ni Mkaguzi wa Jeshi la Polisi kutoka Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Mtandao kwa kufanya doria katika mitandao ya kijamii, PF22863 John Kaaya (45).
Baada ya Lissu kuhitimisha, Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga alimuuliza kwa uchache shahidi maswali ya kusawazisha maswali ya dodoso kwa yale ambayo yalihitaji ufafanuzi zaidi, hivyo baada ya kuhitimisha walidai wapo tayari kuendelea na shahidi namba tatu.
Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tawabu issah, Samweli alidai yeye ni Ofisa wa Polisi wa Jeshi la Polisi Tanzania, kutoka katika Kitengo cha picha Kamisheni ya uchunguzi wa sayansi jinai makao makuu Dar es Salaam, akidai kufanya kazi hiyo kwa muda wa miaka 12 sasa.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow ITV Tanzania RadioOneStereo