
Hamas iliwaachilia mateka 20 wa mwisho walio hai Oktoba 13, lakini hadi sasa imerejesha tu miili tisa kati ya 28 ya waliofariki huko Gaza. Hii ni idadi ndogo sana kwa Israel, ambayo inaongeza shinikizo, anaripoti mwandishi wetu maalum mjini Jerusalem, Aabla Jounaidi. Siku ya Jumatano, mabaki ya mwanamke wa mwisho aliyetekwa nyara, Inbar Hayman, na yale ya afisa Mohamad al-Atrash yalirudishwa. Lakini kwa Israel, kasi ya kurudisha miili ya mateka walioshikiliwa huko Gaza ni ndogo mno.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Jumatano hii, Oktoba 15, Hamas ilitangaza kwamba hawa ndio mateka wa mwisho ambao “imeweza kuwafikia” na kwamba shughuli zilizosalia za miili 19 iliyobaki zinahitaji muda na vifaa ambavyo hawana. Lakini Israel haiamini hili na inaongeza shinikizo, ikiungwa mkono na Donald Trump.
Rais wa Marekani amesema kwenye CNN kwamba anaweza kuidhinisha Israel kuanza tena operesheni za kijeshi huko Gaza ikiwa Hamas itakataa kuheshimu makubaliano ya kusitisha mapigano. Waziri wa Ulinzi wa Israel aliagiza jeshi kuandaa mpango wa “kuingamiza kabisa Hamas huko Gaza.” Zaidi ya maneno, hatua zitazungumza kama awamu hii ya kwanza ya makubaliano bado iko inatekelezwa.