
Baadhi ya bidhaa zinazouzwa nje kwa wingi ni mashine, vyuma, bidhaa za nishati, bidhaa za umeme, plastiki, na vyakula—hasa unga na mafuta. Bidhaa zinazoagizwa kutoka nje zinaangazia nishati, kakao, kilimo, na madini.
Nail Olpak anasisitiza umuhimu wa kuangazia soko la Afrika, ikiwemo mipango ya usafiri, ufikiwaji wa fedha, na Makubaliano mapya ya Biashara Huru.
Tayari, Uturuki ina makubaliano ya Biashara Huru (FTA) na Misri, Tunisia, Morocco, na Mauritius. Makubaliano na Sudan, Ghana, Cameroon, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yako katika hatua ya majadiliano.
Kwa uhalisia, Uturuki inawekeza —siyo tu kwa biashara.
Uwekezaji wake wa moja kwa moja umepita dola bilioni 10. Wajenzi wa Uturuki wamekamilisha miradi zaidi ya 2,000, wenye yenye gharama ya doola bilioni 97 —kutoka viwanja vya ndege na barabara hadi hospitali na ujenzi wa nyumba.
Na yote imeunganishwa. Shirika la ndege la Turkish Airlines sasa inasafiri hadi katika mataifa 51 nchi za Afrika zikiwa 39. Uturuki pia una balozi 44 kote barani Afrika —kutoka balozi 12 mwaka 2002.
Ongeza kwa hilo kazi ya shirika la TİKA, Wakfu wa Maarif, na Taasisi ya Yunus Emre, na hivyo picha inakuwa wazi: Uturuki haijengi tu njia za biashara, lakini pia kujenga uaminifu na miunganisho ya watu.
Jukwaa la TABEF mwaka huu limeweka mkazo katika kilimo na usalama wa chakula, nishati ya kijani na mbadala, madini na maliasili, vifaa na usafiri, teknolojia ya kidijitali, ujenzi na miundombinu, ulinzi na tasnia ya hali ya juu.
Mikutano kati ya wafanyabiashara (B2B) na kati ya serikali na wafanyabiashara (G2B) ilifanyika pamoja na mijadala ya jopo na vikao vya mikutano, ikitoa fursa adimu ya mashirikiano ya ana kwa ana kati ya wadau wa Kiafrika na Kituruki.
Kwa hiyo, Uturuki na Afrika zinaweka malengo makubwa: dola bilioni 40 katika biashara ifikapo 2026, dola bilioni 50 muda mfupi baadaye na maono ya ujasiri ya dola bilioni 75 katika miaka ijayo.