,

Chanzo cha picha, Reuters

Waziri Mkuu mstaafu wa Kenya hayati Raiala Odinga amewahi kuwa na raia wa Tanzania kwa miaka mitatu.

Odinga ambaye alifariki jana asubuhi nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu alipewa uraia na hati ya kusafiria (pasipoti) ya Tanganyika, sasa Tanzania mwaka 1962 na rais wa kwanza wa taifa hilo hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Pasipoti hiyo ilimuwezesha Odinga kusafiri na kwenda Ulaya kwa masomo yake ya juu na Chuo Kikuu.

”Nilitoka nje ya nchi kwa kutumia pasipoti ya Tanzania mwaka 1962 kwenda Ulaya kwa masomo ya shule ya upili,” alisema Odinga akisimulia jinsi Serikali ya Kikoloni nchini Kenya wakati huo ilivyomnyima hati hiyo.

Raila alisema hayo katika moja ya sherehe ya harusi aliyowahi kuhudhurina nchini Tanzania miezi mmine iliyopita yeye akiwa kama mgeni mualikwa.

Kanda inayomuonyesha Raila akizungumzia tukio hilo imesambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii baada ya kifo chake.

Raila amesimulia jinsi yeye na baba yake mzazi Jaramogi Oginga Odinga walivyosariri kwa basi kutoka Niarobi hadi Dar es Salaam katika safari iliyodumu kwa saa 24.

Walipofika anasema walipokewa na kupelekwa katika hoteli moja kwa mapumziko kabla ya kukutana na Mwalimu Julius Nyerere siku iliyofuata ambapo alimsaidia kupata cheti cha usafiri kilichomwezesha kusafiri Ulaya kwa masomo.

”Mwalimu alinipokea kama mtoto wake na kuamuru nipewe pasipoti,” alisema Raila.

Kiongozi huyo alianza safari yake kuelekea Ulaya kutoka jijini Dar es Salaam na kupitia Nairobi kabla ya kuelekea Ujerumani.

Safari ya elimu

Hayati Raila Odinga alisomea shule ya msingi ya Muungano ya Kisumu na shule ya msingi ya Maranda huko Bondo na baadaye kujiunga na Shule ya Upili ya Maranda ya enzi za ukoloni.

Mnamo 1962, akiwa na umri wa miaka 17, baba yake alimpeleka Ujerumani kwa elimu ya juu.

Ukuruba wa baba yake Mzee Jaramogi falsafa za Kisovieti zilifungua milango ya ufadhili wa masomo katika Kambi ya Mashariki.

Raila alisomea katika Taasisi ya Herder, Chuo Kikuu cha Leipzig, akijishughulisha na masomo ya lugha ya Kijerumani.

Mnamo 1965, alihamia Chuo Kikuu cha Ufundi huko Magdeburg ambayo (sasa Chuo Kikuu cha Otto von Guericke), ambako alisomea uhandisi na kuhitimu mwaka 1970.

Alisomea Berlin mashariki enzi ya vita baradi, lakini pia alifanikiwa kuzuru eneo la Berlin magharibi.

Alirejea nchini Kenya mwaka huo huo wa 1970 na kuanzisha kampuni ya kutengeneza vifaa vya ujenzi ambay baadaye aliibadilisha kuwa ya kambuni ya kutengeneza mitungi ya gesi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *