Katika jitihada za kupunguza gharama kwa watumiaji wa nishati na kulinda mazingira kutokana na uzalishaji wa hewa ukaa, Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kupitia ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU), inatarajia kuzindua Viwango Fanisi vya Chini vya Nishati (MEPS) pamoja na maabara za upimaji wa ufanisi wa nishati.
Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa maabara hiyo ni kuhakikisha kuwa vifaa vinavyotumika nchini vinatumia nishati kwa ufanisi.
#AzamTVUpdates
✍Upendo Michael
Mhariri | John Mbalamwezi