
Chanzo cha picha, YASUYOSHI CHIBA/AFP/Getty Images
Kenya bado
iko kwenye majonzi kufuatia kifo cha Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila
Odinga, ambaye aliaga dunia akipata matibabu nchini India.
Mwili wa Raila
Odinga utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) leo
saa tatu na nusu asubuhi kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya kutoka Mumbai,
India.
Siku ya Alhamisi, Oktoba 16, 2025
Rais William
Ruto anatarajiwa kuongoza maafisa wa serikali katika kupokea mwili huo ambao utapelekwa
hadi chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee kuandaliwa.
Mwili wa Raila
kisha atapelekwa katika majengo ya bunge. Na wananchi wataruhusiwa kuutazama
kuanzia kuanzia saa sita mchana hadi kumi na moja jioni na kurejeshwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti cha Lee.
Siku ya
Ijumaa, Oktoba 17, 2025
Mwili wa Raila Odinga utapelekwa katika uwanja wa
michezo wa Nyayo na raia wataweza kutoa heshima zao za mwisho kuanzia saa mbili
asubuhi.
Baadaye,
mwili utarejeshwa nyumbani kwake Karen mjini Nairobi.
Siku ya
Jumamosi, Oktoba 18, 2025
Mwili wa Raila Odinga utaondoka Nairobi kuelekea kaunti
ya Kisumu.
Wananchi
watakuwa na fursa ya kuutazama katika uwanja wa Jomo Kenyatta Grounds, Kisumu,
kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa tisa mchana.Na mwili huo
utaondoka kutoka mji wa Kisumu hadi Bondo, kaunti ya Siaya.
Jumapili,
Oktoba 19, 2025
Ibada ya
mazishi na shughuli za maziko, zitafanyika Bondo, kaunti ya Siaya kuanzia saa
tatu asubuhi.
Pia unaweza kusoma: