MWANZO wa taratibu aliokuwa nao beki wa kushoto wa Yanga, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ umemwibua baba yake mzazi, Hussein Mohamed Sr anayeona ameanza vizuri na anamtabiria atafanya makubwa katika klabu hiyo.

Mohamed Sr amesema anatambua siyo jambo jepesi kuanza kucheza kikosi cha kwanza Yanga kama ilivyokuwa Simba na Tshabalala alikuwa panga pangua, lakini kitendo cha Kocha Romain Folz kumpa nafasi katika mechi nne kinampa nafasi ya kupambania namba.

TSHABAL 05

Beki huyo alijiunga na Yanga dirisha kubwa la usajili msimu huu akitokea Simba ambako alicheza kuanzia mwaka 2014 hadi 2025.

Tshabalala anapambania nafasi na Chadrack Boka ambaye amekuwa na kikosi hicho tangu msimu uliopita akiwa tegemeo.

TSHABAL 01

Uamuzi wa Tshabalala kutua Yanga baada ya kumaliza mkataba wake Simba, baadhi ya mashabiki walikiona kitendo hicho ni kama anakwenda kumalizia soka lake wakimuita mzee, lakini baba yake amefafanua hilo akisema wengi wana tabia ya kuwachoka wachezaji wazawa kama ilivyo kwa Shomari Kapombe wa Simba.

“Mfano mzuri ni Kapombe, mara kadhaa Simba ilitaka kumwacha kwa kumuona mzee, ila ajabu kila beki anayekuja kumpa changamoto ya ushindi hawezi kumweka benchi, ndivyo ilivyo kwa Tshabalala, kikubwa ni wachezaji kutambua majukumu yao.

TSHABAL 02

“Niliona baadhi ya mashabiki waliokuwa wanamuona ni mzee anakwenda Yanga kumalizia soka, mechi alizocheza na alichokionyesha kitakuwa kimewapa majibu ya mitazamo yao, kikubwa aendelee kupambana kwa ajili ya timu iliyomuajiri,” amesema mzee huyo.

Aidha, Mohamed Sr amesema: “Natambua siyo kazi rahisi Tshabalala kwenda Yanga na kuanza moja kwa moja kikosi cha kwanza, kwani beki ya kushoto yupo Chadrak Boka tangu amejiunga na timu kiwango chake ni kizuri, ninachofurahia ushindani wa namba ukiwa mkubwa ndiyo mafanikio ya klabu kushinda.

TSHABAL 03

“Mimi ni mwanachama wa Yanga, nawaunga mkono wachezaji wote, kikubwa ni klabu ifikie mafanikio yake, naamini kabisa wakishindana pia wanapandisha viwango vyao kuwa bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *