
Katika kipindi ambacho maji safi yana thamani zaidi kuliko hapo awali, mifumo bora ya kutibu maji ya ‘Reverse Osmosis (RO)’ imekuwa chaguo muhimu na sahihi kutokana na kutumia mbinu za kisasa za kutibu maji.
Hata hivyo mifumo hiyo inaweza kushindwa kufanya kazi ipasavyo kama haitatunzwa vizuri.
Matumizi ya kemikali zisizo na ubora yanaweza kusababisha gharama kubwa za umeme na kupunguza ufanisi wa mifumo jambo linalochangia kuongezeka kwa gharama za kutibu maji.
Ili kukabiliana na changamoto hii, Davis & Shirtliff, kampuni inayoongoza Tanzania na ukanda wa Afrika Mashariki katika kutoa suluhu za kisasa za maji na nishati kwa kushirikiana na H2O Innovation Ltd (Genesys) wamekuja na kemikali maalumu zinazoiwezesha mitambo ya RO kufanya kazi kwa ufanisi na kwa uendelevu.
Umuhimu wa kutumia kemikali sahihi
Kutumia kemikali sahihi sio tu kutakusaidia kuepuka matengenezo ya mara kwa mara, bali ni uwekezaji wa muda mrefu katika utendaji kazi wa mifumo ya kutibu maji.
Uchaguzi sahihi wa kemikali unasaidia kuboresha utendaji kazi wa mifumo, kupunguza gharama za umeme, kupunguza hali ya kutibu maji mara kwa mara na hivyo kudumisha ubora wa maji.
Kutumia kemikali sahihi kunaweza kuokoa hadi asilimia 30 ya gharama za uendeshaji huku kukiongeza ufanisi na kupunguza upotevu wa maji.
Kutumia kemikali sahihi kuna faida nyingine ikiwemo kusaidia mifumo kufanya kazi kwa muda mrefu na kuzuia uharibifu wa mara kwa mara na hivyo kupunguza matengenezo yanayoongeza gharama za uendeshaji.
Kemikali sahihi pia huboresha ufanisi wa matumizi ya umeme kwa sababu mfumo hutumia kiasi kidogo cha shinikizo. Zaidi ya hayo, matumizi bora ya kemikali yanahakikisha ubora wa maji ambalo ni jambo muhimu katika shughuli za viwanda kama vile vya kuzalisha dawa na usindikaji wa chakula ambako viwango huzingatiwa zaidi.
Suluhu sahihi kwa kila changamoto ya RO
Ushirikiano wa Davis & Shirtliff na H2O Innovation Ltd (Genesys) umewezesha kupatikana kwa suluhu mbalimbali zinazosaidia kutatua changamoto za mfumo wa RO.
Miongoni mwa suluhu hizo ni kemikali za ‘antiscalants’ kama vile Genesys LF, ambayo hutoa ulinzi dhidi ya chembechembe za kioganiki kwenye maji na Genesys SI, iliyoundwa mahsusi kwa ajili ya kutibu maji yenye Silica nyingi ambapo kemikali za kawaida mara nyingi hushindwa.
Ili kuwezesha haya, kuna aina mbalimbali za kemikali za kusafisha maji (CIP) ambazo hutoa usafishaji wa kina na ulinzi wa muda mrefu. Genesol 704 (pH ya juu) ni kisafishaji ambacho huondoa uchafu wa kikaboni, ikijumuisha vijidudu kama vile bakteria, kuvu na mwani kwa kutumia teknolojia ijulikanayo kama ‘micro-bubble’. Genesol 38 (pH ya chini) ni kisafisha maji ambacho kinalenga kuondoa kiwango cha Inorganic na chembechembe za chuma.
Genesol 80 hufanya kazi ya kuondoa vijidudu na kuua bakteria ili kuboresha utendaji kazi wa mfumo wa kutibu maji. Kwa pamoja, bidhaa hizi huhakikisha kwamba mfumo wa RO unabaki kuwa salama, bora na wa kuaminika katika shughuli zake za kila siku za uendeshaji.
Kuongeza ufanisi wa ROI kwa kutumia kemikali za kisasa
Matumizi sahihi ya kemikali yanaweza kuleta tofauti inayoweza kupimika katika utendaji na gharama. Davis & Shirtliff wanaeleza kwamba, antiscalants bora zinaweza kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za matengenezo.
Kemikali bora pia hupunguza shinikizo la mfumo, kupunguza matumizi ya umeme. Kwa kuongezea, uchaguzi sahihi wa kipimo cha kemikali unaweza kupunguza matumizi ya kemikali na hivyo kuleta faida ya ufanisi huku ikipunguza upotevu wa kemikali hiyo.
Mapinduzi kama haya yanatafsiri moja kwa moja juu ya faida ya haraka kwenye uwekezaji.
Ushirikiano wenye faida
Kinachotofautisha Davis & Shirtliff sio tu ubora wa bidhaa zake lakini huduma zake baada ya mauzo. Kampuni hiyo inatumia uchambuzi wa kina ili kubaini aina na kipimo bora cha kemikali kwa kila mfumo mahususi wa RO ili kuhakikisha ufanisi na kupunguza upotevu wa kemikali. Pia hudumisha usambazaji wa kemikali ili kuzuia usumbufu na gharama za uendeshaji unaosababishwa na upungufu wa kemikali.
Zaidi ya usambazaji wa bidhaa, Davis & Shirtliff inatoa usaidizi wa kiufundi wa mara kwa mara, matengenezo na utatuzi wa matatizo ili kuwasaidia wateja wake kufikia malengo ya biashara zao.
Ushirikiano huu unahakikisha kwamba wateja wanapokea sio tu suluhu bora za kemikali bali pia usaidizi endelevu unaolinda uwekezaji wao. Muhimu pia ni msisitizo wa kampuni juu ya uendelevu, kuongeza uwajibikaji katika matibabu ya maji ambayo huongeza ufanisi wa mfumo huku ukipunguza athari za mazingira.
Kampuni ya kuaminika katika suluhu za maji
Kwa biashara zinazotegemea ubora wa maji, mfumo wa RO ni rasilimali muhimu ambayo lazima ilindwe ili kuhakikisha inafanya kazi kwa ufanisi na kwa muda mrefu. Kwa kutumia ubunifu wa wataalam wa Davis & Shirtliff na utendaji kazi imara wa kemikali za Genesys, waendeshaji wa mitambo na viwanda wanaweza kuwa na imani kwamba mifumo yao itaendelea kutibu maji kwa ubora, ufanisi na uendelevu.
Ahadi ya Davis & Shirtliff ni “majisafi, utendaji kazi bora na ushirikiano.”