Nchini Madagascar, jeshi linaimarisha mamlaka yake mpya siku mbili baada ya tangazo lake mbele ya ikulu ya rais huko Ambohitsorohitra. Kanali Randrianirina ataapishwa siku ya Ijumaa Oktoba 17 kuwa rais wa Madagascar, kwa mujibu wa taarifa iliyotiwa saini naye na kutangazwa Jumatano jioni, Oktoba 15, kwenye ukurasa wa Facebook wa televisheni ya taifa ya Madagascar. Sherehe hiyo imepangwa kufanyika huko Antananarivo.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kanali Randrianirina ataapishwa kama rais wa Jamhuri ya Madagascar siku ya Ijumaa katika Ikulu ya rais ya Ambohidahy, makao makuu ya Mahakama Kuu ya Katiba, anaripoti mwandishi wetu huko Antananarivo, Guilhem Fabry. Kiongozi huyo mpya wa Kisiwa hiki Kikubwa alitangaza kuvunjwa kwa taasisi hii siku ya Jumanne alasiri baada ya kuchukua mamlaka, kabla ya taasisi hiyo, katika uamuzi uliochapishwa saa moja baadaye, kumtaka kuchukuwa madaraka kama Mkuu wa Nchi.

Mabadiliko ya kauli yalibainishwa katika taarifa iliyotiwa saini na Kanali Randrianirina, iliyochapishwa siku ya Jumatano jioni: Baraza jipya la Rais linazingatia uamuzi wa Mahakama Kuu ya Katiba. Taarifa chache bado zimetolewa kuhusiana na kikao rasmi cha kuapishwa kitakachofanyika siku ya Ijumaa.” Mnamo mwaka 2023, Andry Rajoelina alichagua uwanja wa Mahamasina na watazamaji wake 40,000 kwa kula kiapo baada ya kuchaguliwa tena.

Kwetu sisi, ni muhimu kuwa na serikali inayokubalika na wote, yenye Waziri Mkuu ambaye anakidhi vigezo tulivyoweka pamoja.

Kwa mujibu wa Hony Radert, Katibu Mkuu wa mungano wa mashirika y kiraia, ni muhimu kufikia makubaliano ya kisiasa ambayo yanajumuisha washikadau wote.

Jaji wa zamani kuiwakilisha Madagascar katika Mashirika ya Kimataifa

Siku ya Jumatano jioni, kulingana na duru za kuaminika, wakili na jjaji wa zamani aliye uhamishoni nchini Ufaransa, Fanirisoa Ernaivo, ameagizwa na Baraza la taifa la Ulinzi wa Mpito, taasisi mpya kabisa, kuiwakilisha Madagascar katika mashirika ya kimataifa ili kuongoza mchakato katika mahakama ya kimataifa juu ya kesi zinazohusisha, hasa, mfanyabiashara mwenye ushawishi mkubwa Mamy Ravatomangantantarivo, anaripoti mwandishi wetu wa habari Sarah Tétaud.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *