Wakati Marekani ikiendelea kushambulia meli katika bahari ya Caribbean, ikizishutumu kuwa ni za wafanyabiashara haramu ya  mihadarati kutoka Venezuela, mvutano kati ya Washington na Caracas unaendelea kuongezeka. Rais wa Marekani Donald Trump hivi punde ameidhinisha CIA kufanya operesheni hatari na za siri nchini Venezuela, Gazeti la New York Times limefichua siku ya Jumatano, Oktoba 15. Caracas amepinga na kutoa wito wa “amani.”

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mbele ya waandishi wa habari katika Ofisi ya Oval, Donald Trump alithibitisha ripoti ya New York Times: rais amewapa CIA idhini, lakini bila kutaja nini cha kufanya, anaripoti mwandishi wetu wa Washington, Vincent Souriau.

Lakini mwandishi wa habari alipomuuliza iwapo Nicolas Maduro, Rais wa Venezuela anaweza kuwa mlengwa wa mauaji yaliyolengwa, Donald Trump alikataa kujibu na kuendeleza mashaka hayo: “Sitaki kujibu swali kama hilo; itakuwa ni upuuzi kwangu kujibu. Lakini nadhani Venezuela inajua mambo yanazidi kuwa moto, na nadhani hivyo ndivyo hali ilivyo kwa nchi nyingine nyingi.”

Bila kumhusisha moja kwa moja na kibali hiki, Donald Trump kisha akarejea kwenye matamanio yake: Magenge ya Venezuela na kile alichoeleza, bila ushahidi, kama utitiri wa watu wasio na utulivu nchini Marekani: “Waliayacha magereza yakitekekezwa kwenye ardhi ya Marekani, waliwasili kupitia mpaka, kwa sababu tulifungua mpaka kwa kila mtu. Waliruhusu maelfu na maelfu ya wafungwa, wagonjwa kutoka kwa wagonjwa wa akili katika nchini Marekani. Na nitawarudisha.” ยป

Hadi sasa, jeshi la Marekani limepeleka angalau meli nane za kivita kwenye Caribbean, pamoja na manowari. Pia ina karibu wanajeshi 10,000 katika eneo hilo.

Nicolas Maduro atoa wito wa “amani” na akosoa “Mapinduzi ya CIA”

Jibu la nchi ya Caribbean kwa shinikizo linaloongezeka lilikuwa la haraka. Rais wa Venezuela Nicolas Maduro alionya kuhusu uwezekano wa vita katika visiwa vya Caribbean, akiwa tayari ameomba mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita.

Rais wa Venezuela alitaka kuongea na mwenzake Donald Trump moja kwa moja wakati wa akionekana siku ya Jumatano, anaripoti mwandishi wetu huko Caracas, Alice Campaignolle. “Hapana kwa mapinduzi yatakayoyochochewa na CIA,” alisema, kabla ya kuanza kwa Kiingereza: “Nisikilizeni, sio vita, amani tu.”

Viongozi wakuu wa nchi hiyo, na Nicolas Maduro kwanza kabisa, kwa sasa ni walengwa wanaowezekana kwa utawala wa Trump, ambao unadai kutaka kupambana na ulanguzi wa dawa za kulevya. Rais mwenyewe anashutumiwa na Washington kwa kuongoza kundi, Cartel de los Soles, na zawadi ya dola milioni 50 imetengwa kwa yule atakayewezesha kupaitkana kwa rais hut ?.

Tangu kuwasili kwa meli za Marekani katika pwani ya Venezuela, Nicolas Maduro amejitahidi kutoa wito wa amani na heshima kwa mamlaka ya taifa, lakini pia amepanga jeshi lake na wafuasi wake kujilinda katika tukio la uvamizi. Mvutano unaendelea kuongezeka nchini humo, ambapo wengi wanatumai kumuona Nicolas Maduro akiondoka madarakani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *