
Mfalme Abdullah II wa Jordan amesisitizia udharura wa kuundwa nchi huru ya Palestina.
Mfalme wa Jordan amebainisha kuwa bila ya kuanzishwa tena mchakato wa amani unaopelekea kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina, eneo la Asia Magharibi litakabiliwa na hatima mbaya.
Mfalme wa Jordan amesema: “Kumekuwa na majaribio mengi ya kutafuta amani hadi sasa, na suluhisho pekee ni kuanzishwa kwa taifa huru la Palestina.” Mfalme wa Jordan aliongeza kuwa hana imani na maneno ya Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel lakini kuna watu Israel ambao watawala wa Kiarabu wanaweza kushirikiana nao katika kuleta amani.
Mwezi uliopita na katika hatua ya kihistoria, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipasisha azimio lililopendekezwa na Ufaransa na Saudi Arabia, na kutangaza kuunga mkono kuanzishwa kwa nchi huru ly Palestina na kutekelezwa njia ya ufumbuzi wa serikali mbili.
Azimio la Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kwa mara ya kwanza kwa upande moja liliunga mkono pakubwa kuundwa nchi huru ya Palestina na katika upande mwingine, liliaashiria kuanzishwa mchakato wa amani wenye itibari kwa ajili ya kutatua kadhia ya Palestina na Israel.
Nchi za Ulaya ambazo kwa miaka kadhaa sasa zinaiunga mkono Israe hivi sasa zimelazimika kuchukua za kivitendo kutokana na chokochoko na hatua za uvamizi za utawala wa Kizayuni na mashinikizo ya fikra za waliowengi duniani.