Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Bara, Mussa Mwakitinya amewasihi wananchi kujitokeza kwa amani tarehe 29 Oktoba kupiga kura na kumpa ushindi wa kishindo mgombea wa urais wa CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wabunge na madiwani wa chama hicho.

Ametoa kauli hiyo akiwa wilayani Nyang’hwale mkoani Geita katika kampeni za kutafuta kura za mgombea urais wa chama hicho.

Amesema amani ndiyo msingi wa maendeleo, ikiwemo shughuli za kiuchumi na kijamii, hivyo wananchi waitunze kama mboni ya macho yao.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *