Mke wa Rais Emine Erdogan alisisitiza kuwa vita, mauaji ya halaiki, mabadiliko ya tabianchi na umasikini bado vinaendelea kuwa masuala ya msingi katika ajenda ya dunia.

“Hakika, dunia inahitaji simulizi mpya,” Bi Erdogan alisema.

“Ninaamini kuwa simulizi hiyo itaandikwa kwa kalamu ya mwanamke. Kila siku, katika kona tofauti ya dunia, mwanamke mmoja anageuza wazo kuwa uhalisia. Kama vile maua yanavyochipuka katikati ya theluji, mawazo haya yanatia matumaini kwa binadamu hata katika mazingira magumu kabisa.”

Akiangazia sifa za uongozi za wanawake, alibainisha kuwa wanawake sio tu hutoa suluhu kwa matatizo ya kimataifa lakini pia wanakuza utamaduni wa amani.

“Vizazi vilotokana mikononi mwa wanawake hufanikiwa kuunda mustakabali mzuri. Hivyo basi, wanawake wanaposhiriki katika maisha ya kiuchumi, hawajiendelezi wao tu bali pia jamii zao.”

Ushirikiano wa uchumi katia ya Uturuki na Afrika

Mke wa Rais Emine Erdogan alisisitiza zaidi ushirikiani kati ya Uturuki na Afrika, akielezea kanda hizo mbili kama wadau muhimu katika uchumi wa dunia.

Hisia ya mwanamke inapochanganywa na uongozi, huibua suluhisho jumuishi linalolinda utu wa binadamu pamoja na mazingira. Dunia inahitaji mkono wa mwanamke katika kila janga la kimataifa, kimazingira na kibinadamu.” Mke wa Rais Emine Erdogan alisisitiza ndiyo maana ninaamini kwa dhati kwamba wanawake wanapaswa kuwa katika nafasi ya msingi katika uhusiano kati ya Uturuki na nchi za Afrika.

Akitaja mara kadhaa alivyotembelea nchi za Afrika kufuatia mpango wa Uturuki kwa Afrika ulioanzishwa mwaka 2005, Mkw wa Rais Eimne Erdogan aliongeza: “Nilipata fursa ya kuzitembelea nchi 30 tofauti. Mara nyingi nilishuhudia kwa macho yangu nguvu ya wanawake wa Kiafrika, busara na bidii yao pamoja na mchango wao kwa jamii zao. Tangu mwanzo, nimekuwa na hamu kubwa ya kushirikiana na wanawake hawa jasiri.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *