Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Ramadhan Kailima, amewakumbusha wananchi na wadau wa siasa nchini umuhimu wa kuzingatia sheria wakati wa kipindi cha uchaguzi, hasa katika masuala yanayohusu uhamasishaji wa wapiga kura.
Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo cha televisheni cha UTV, Kailima amesema Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024, kifungu cha 129, kinaeleza kuwa si sahihi kutumia nguvu, vitisho, au udanganyifu kumshawishi mtu asishiriki kupiga kura.
Ameeleza kuwa kifungu hicho kinakataza vitendo vyovyote vya vurugu au hila vinavyolenga kumshawishi mpiga kura kupiga au kuacha kupiga kura.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates