Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Makame, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, akisisitiza kuwa maamuzi yao ndiyo yatakayoweka msingi wa ndoto na hatma ya watoto wao walioko shuleni.

Makame alitoa wito huo mjini Tunduma wakati wa ziara maalum ya “Operation October 29”, yenye lengo la kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji kura.

Amesema ataendelea na ziara hiyo katika halmashauri zote tano za Mkoa wa Songwe kuhakikisha kila mwananchi anatimiza wajibu wake wa kikatiba.

Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Songwe, SACP Augustino Senga, amewahakikishia wananchi ulinzi na usalama wa kutosha siku ya uchaguzi, huku akitoa onyo kwa yeyote atakayejihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani.

✍ Joyce Lyanda
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *