Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya CRDB, Profesa Neema Mori amewakaribisha wawekezaji wa kimataifa kuchangamkia fursa za kiuchumi zilizopo Tanzania na katika Ukanda wa Afrika Mashariki, huku akiwahakikishia kupata ushirikiano madhubuti kutoka benki hiyo.

Akizungumza kando ya Mkutano wa Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) unaoendelea jijini Washington, Marekani, Profesa Mori amesema Benki ya CRDB imejipambanua kama daraja kati ya mitaji ya kimataifa na masoko yanayokua kwa kasi barani Afrika, ikijivunia uzoefu mkubwa wa kuhudumia Tanzania, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

“Tunaona fursa kubwa katika Ukanda wa Afrika Mashariki,” alisema Profesa Mori, akibainisha kwamba CRDB imejipanga kuwa mwezeshaji mkuu wa uwekezaji katika sekta za madini, utalii, viwanda na kilimo — ambazo ni injini kuu za ukuaji wa uchumi wa bara la Afrika.

Amesisitiza kuwa uwezo wa kifedha, mtandao mpana wa kikanda, na mifumo imara ya kidijitali ya CRDB vinatoa uaminifu na usalama wanaoutaka wawekezaji wanapotafuta mshirika wa benki thabiti ndani ya Afrika Mashariki na Kati.

✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *