NAIBU WAZIRI HAMIS MWINJUMA AWATAKA WATANZANIA KKUISAPOTI DAR CITY

NAIBU WAZIRI HAMIS MWINJUMA AWATAKA WATANZANIA KKUISAPOTI DAR CITY

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma, ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu ya kikapu ya Dar City katika mashindano ya Kimataifa (Road to Bal) yatakayozinduliwa Ijumaa, Oktoba 17, 2025.

Akizungumza wakati wa maandalizi ya mashindano hayo, Mwinjuma amesema amefurahishwa na hatua ya Tanzania kuunda timu ya kikapu inayojumuisha wachezaji kutoka ndani na nje ya nchi, hatua aliyoeleza kuwa inaonyesha maendeleo ya michezo nchini na mchango mkubwa wa wachezaji hao katika kukuza sifa za taifa kimataifa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ameipongeza timu ya Dar City kwa uwekezaji mkubwa walioufanya, ikiwemo usajili wa kocha na wachezaji wa kigeni wenye uzoefu wa kimataifa.

Aidha, kutokana na mchezo wa kikapu kutokuwa na mashabiki wengi nchini, Chalamila aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) ambako mashindano hayo yatafanyika, ili kushuhudia burudani na ushindani wa kiwango cha juu unaotarajiwa.

Mhariri @claud_jm
#AzamTvSports

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *