Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeendelea na zoezi la kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi rasmi kupitia kliniki maalum za ardhi zinazoendelea nchini.

Katika Kliniki ya Ardhi inayoendelea Kata ya Muriet, jijini Arusha, jumla ya viwanja 18,886 vimetambuliwa huku viwanja 14,562 vikiidhinishwa kupatiwa hati milki.

Mratibu wa Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha, Elia Kamihanda, amesema hatua hiyo inalenga kuongeza kasi ya umilikishaji na kuwahakikishia wananchi usalama wa milki zao.

Kliniki hizo pia zinatoa elimu ya matumizi ya mfumo wa e-ardhi, kutatua migogoro ya ardhi, na huduma zinatarajiwa kufanyika pia Chalinze, Nzega, Mbarali, Njombe, Mtwara na Peramiho.

Mharirir @claud_jm
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *