Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imewakumbusha wakulima kote nchini kujisajili kwenye mfumo wa ruzuku ya mbegu bora, ili kunufaika na mpango wa serikali wa kuongeza tija katika kilimo.
Mkurugenzi wa Tathmini na Majaribio wa TOSCI, Matengia Swai, amesema wakulima watakaonunua mbegu zisizothibitishwa wanakiuka sheria, na akawataka wazalishaji na wauzaji wa mbegu kuhakikisha wanajisajili kisheria kabla ya kufanya biashara.
Mhariri @moseskwindi