.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester City wanapanga dau la pauni milioni 75 kumnunua kiungo wa kati wa Nottingham Forest Elliot Anderson msimu ujao wa joto lakini kuna uwezekano wakakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa Chelsea kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza, 22. (Express)

Tottenham wanajiandaa kuchukua hatua kali ya kumrejesha Harry Kane kaskazini mwa London kutoka Bayern Munich msimu ujao wa joto na wako tayari kutimiza masharti ya kutolewa kwa nahodha huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 32 na mahitaji ya mshahara. (TeamTalks,)

Crystal Palace wametulia kuhusu mustakabali wa Adam Wharton huku kukiwa na uvumi unaoongezeka kutoka kwa wapinzani wa Premier League Manchester United kutaka kumnunua kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)

Kocha mkuu wa Chelsea Enzo Maresca ana mashaka juu ya mustakabali wake wa muda mrefu Stamford Bridge huku Juventus ikimfikiria Muitaliano huyo mwenye umri wa miaka 45 kama mgombea makini wa kuinoa klabu hiyo ya Serie A. (TeamTalks)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji katika msimu wa joto na wanamlenga Mateo Retegui, huku Ruben Amorim akiwa tayari kutumia hadi £52m kumsajili mshambuliaji huyo wa Italia mwenye umri wa miaka 26 kutoka klabu ya Saudi Pro League Al-Qadsiah. (Fichajes – In Spanish)

Mshambuliaji wa Uturuki Kenan Yildiz anaendelea kushinikiza kuboreshwa kwa kandarasi katika klabu ya Juventus lakini huku mazungumzo yakiwa bado hayajazaa matunda., vilabu vikiwemo Chelsea, Arsenal na Barcelona vinamfuatilia kwa karibu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Gazzetta dello Sport – In Italy)

Paris St-Germain wanafanya mazungumzo ya mkataba na Bradley Barcola, 23, baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kuvutia vilabu kadhaa vikiwemo Liverpool na Bayern Munich . (L’Equipe – In French)

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Barcelona na Real Madrid wako tayari kupigana vikumbo kumsajili beki wa Bayern Munich Dayot Upamecano, 26, kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao lakini Manchester United pia wanavutiwa na mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa. (Footmercato – In French)

AS Roma wako katika nafasi nzuri ya kumsajili fowadi wa Manchester United Joshua Zirkzee lakini Como pia ina ufadhili wa kumrejesha mshambuliaji huyo wa Uholanzi, 24, kwenye Serie A. (Gazzetta dello Sport – In Itali).

Juventus wamekanusha maswali mengi kuhusu kiungo wa kati wa Ufaransa Khephren Thuram, 24, kutoka klabu za Premier League zikiwemo Arsenal, Chelsea na Liverpool katika kipindi cha miezi sita iliyopita. (TBR Football, nje)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *