London, England. Kocha wa timu ya taifa ya England, Thomas Tuchel ameweka wazi kwamba atakaa kikao na staa wa Real Madrid,  Jude Bellingham kujadili mustakabali wake katika kikosi cha timu hiyo.

Kiungo huyu aliachwa nje ya kikosi cha England kwa mechi mbili dhidi ya Wales na Latvia, ingawa anatarajia kurejea mwezi ujao kwa michezo ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Serbia na Albania.

Bellingham alikosa mechi za Septemba dhidi ya Andorra na Serbia kutokana na upasuaji wa bega, lakini licha ya kucheza mechi tano akiwa na Real Madrid, alishangaza wengi baada ya kuachwa nje ya kikosi kilichoitwa kucheza mechi za kimataifa katika kalenda iliyopita.

TUCHE 01

Alipoulizwa kama atazungumza na Bellingham, Tuchel alisema: “Nadhani nitaongea naye, kwa nini isiwe hivyo? Ni mchezaji muhimu na mkubwa. Pia nitaongea na wachezaji wengine ambao hawajaitwa kambini. Kutokuitwa kwao sio kwa sababu wamefanya kosa lolote. Hii siyo adhabu ni utaratibu wa kawaida, wachache nilioongea nao kila mmoja alionyesha nia ya kutamani kurejea.

“Lakini naona huwa tunazungumza kuhusu majina machache sana ambayo hayajaitwa, tunasahau kuna mastaa kama Conor Gallagher, Trevoh Chalobah, na Cole Palmer ambao ni majeruhi lakini nao walipaswa kuwa nasi hapa kutokana na viwango vyao.”

Hata hivyo, hakuna uhakika kuhusu nafasi ya Bellingham katika kikosi hicho, hali inayozidi kuonyesha huenda Tuchel hana mpango wa kumtumia.

TUCHE 02

Tuchel amejikuta katika hali ngumu baada ya kutoita baadhi ya wachezaji ambao wadau wengi wanaeleza wanatakiwa kuwamo.

Miongoni mwa wachezaji hao mbali ya Bellingham pia yupo Phil Foden na Jack Grealish ambao hawajajumuishwa kabisa katika kikosi hivi karibuni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *