Wakimbizi wa Burundi wanaoishi katika kambi ya Nyarugusu mkoani Kigoma wamefutiwa rasmi hadhi ya ukimbizi na kutakiwa kurejea Burundi hadi kufikia Juni mwakani kabla ya hatua kuanza kuchukuliwa dhidi yao itakapofika Julai 2026.
Taarifa ya kufutwa kwa hadhi hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Huduma ya wakimbizi nchini, Sudy Mwakibasi wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Jacob Ruvilo ana maelezo zaidi.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi