Wanajeshi nchini Kenya wamelazimika kufyatua risasi hewani kutawanya umati wa watu uliokuwa umefurika nje ya uwanja wa Kasarani jijini Nairobi, wakati msafara uliobeba mwili wa Raila Odinga ukiwasili.
Umati huo ulikuwa umesongamana katika lango kuu la uwanja huo huku wengi wakijaribu kuingia ndani licha ya ulinzi mkali uliowekwa.
Baada ya muda, hali ilidhibitiwa na maandalizi ya kuuaga mwili wa Odinga yakaendelea kwa utulivu.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi