Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania wafanya ukaguzi wa mbolea katika mkoa wa ruvuma na kutoa angalizo kwa mawakala kuelekea msimu mpya wa kilimo 202526.
Ukaguzi uliofanyika umeleka kubaini utoshelevu wa mbolea, ubora wa mbolea zinazopelekwa kwa wakulima pamoja na kuzungumza na mawakala kuwakumbusha kufuata sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Mkoa wa Ruvuma unatajwa kuongoza kitaifa kwa zaidi ya miaka sita katika uzalishaji wa mazao ya chakula huku afisa kilimo akiahidi kuendelea kusimamia vema sekta hiyo ili wakulima wapate mbolea zenye ubora ili wasipate hasara.
Mkoa wa ruvuma unatajwa kutumia tani laki moja na elfu sita katika msimu uliopita, hata hivyo bado wanataraji kutumia zaidi ya tani 127,000 katika msimu huu kutokana na mwamko mkubwa wa wakulima kutumia mbolea ili kuongeza uzalishaji.
Na, @dkhan1410
@habaristartv