YANGA SAFARINI: Kikosi cha Yanga kimeondoka Dar es Salaam mapema asubuhi ya leo kwenda Malawi kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa r...

YANGA SAFARINI: Kikosi cha Yanga kimeondoka Dar es Salaam mapema asubuhi ya leo kwenda Malawi kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, Silver Strikers Oktoba 18, Uwanja wa Taifa wa Bingu, Lilongwe Malawi.

Kocha mpya Msaidizi wa Yanga, Mmalawi Patrick Mabedi ni miongoni mwa waliosafiri na timu ikiwa ni wiki moja tangu ajiunge na kikosi cha Wananchi kuliongezea nguvu benchi la Ufundi chini ya Kocha Mkuu, Mfaransa, Romain Folz.

Timu hizo zinatarajiwa kurudiana Oktoba 25 Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

#YangaSC #CAFCL

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *