Guterres amesema “mara nyingi watu wanaoishi katika umasikini wanalaumiwa, wana nyanyapaliwa na kuwekwa mbali lakini umasikini sio kushindwa kwa mtu binafsi, ni kushindwa kwa kimfumo na mtu kunyimwa utu na ubinadamu”

Dunia ikiadhimisha siku hii Guterres amekumbusha kuwa itumike kwa watu wote kukomesha unyanyasaji wa kijamii na kitaasisi kwa watu wanaoishi katika umaskini na kuheshimu ahadi ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya kutokomeza umaskini katika aina zake zote, kila mahali.

Ili kutimiza hilo Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema “zinahitaji sera ambazo hazimuachi mtu nyuma: huduma za afya na nyumba za bei nafuu; kazi nzuri na ujira wa haki; ulinzi wa kijamii kwa wote; uhakika wa chakula; elimu bora; na ufadhili unaofanya kazi kwa nchi na jamii.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *