#HABARI: Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, imewakamata Watanzania 79 wanaojihusisha na biashara ya kuingiza Wahamiaji haramu nchini, pamoja na raia wa kigeni zaidi ya 2000 walioingia na kuanza kuishi kinyume cha sheria ambao wanatoka katika mataifa mbalimbali yakiwemo ya Jumuiya za Africa Mashariki na Ulaya kisha kurejeshwa makwao.
Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Kagera, Kamishina Msaidizi wa Idara hiyo, Petro Malima amesema raia hao wa kigeni wamekamatwa katika msako uliofanyika kwa kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba nane mwaka huu.
Katika hatua nyingine kamishina huyo msaidizi wa idara ya uhamiaji mkoani Kagera Petro Malima, amewaonya raia wa kigeni kutoingilia uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 29 mwaka huu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.