#HABARI: Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, pamoja na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, leo wameungana na viongozi mbalimbali duniani kutoa heshima zao za mwisho kwa Hayati Raila Odinga katika ibada ya kitaifa iliyoandaliwa katika Uwanja wa Nyayo, jijini Nairobi.

Wakiwa sehemu ya ujumbe rasmi kutoka Tanzania, viongozi hao wameelezea masikitiko yao kwa kuondokewa na mmoja wa wanamapambano mashuhuri wa Afrika, wakimtaja Raila kama mwanasiasa shupavu, mzalendo wa kweli na nguzo ya demokrasia barani Afrika.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango alitoa salamu za pole kwa familia ya Raila, Serikali na wananchi wa Kenya kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na wananchi wa Tanzania. Alisema, “Afrika imepoteza kiongozi wa kizazi cha mabadiliko.”

Viongozi hao waliungana na maelfu ya wananchi waliofurika uwanjani kutoa heshima zao za mwisho, huku maandalizi ya safari ya mwisho ya Raila Odinga kuelekea kijijini kwake Bondo yakiendelea. Maziko ya Kitaifa yanatarajiwa kufanyika Jumamosi, Oktoba 19, 2025.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *