#HABARI: Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), katika Jimbo la Peramiho, Bi.Jenista Mhagama, ametoa rai kwa wananchi kuilinda amani na utulivu uliopo kwakuwa ndio kichocheo kikubwa cha maendeleo nchini.
Amezungumza katika Kijiji cha Lusonga Kata ya Magagura ikiwa ni muendelezo wa kampeni zake za kupita kila Kijiji ndani ya Jimbo, kunadi Sera za CCM kupitia ilani ya uchaguzi wa chama hicho na kuomba wananchi kukipigia kura za ndio kwa wagombea wa CCM katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Ameongeza kuwa ili nchi iendelee inahitaji uongozi ulio bora, siasa makini na safi na vitu hivi vimeasisiwa na chama cha Mapinduzi tangu wakati wa TANU hivyo amewahimiza wananchi wote ifikapo Oktoba 29, 2025 wahakikishe wanapiga kura ili kuchagua viongozi bora kutoka CCM kwakuwa ndio wenye uwezo wa kuendelea kudumisha amani na utulivu kwa wananchi wote.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.