#HABARI: Mjadala mzito umeibuka baada ya shahidi wa tatu katika kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu kuomba Mahakama impatie kompyuta ili aweze kuhakiki vielelezo vilivyoletwa Mahakamani ni vile alivyofanyia uchunguzi.
Baada ya shahidi huyo Inspekta Samweli Elibariki Kaaya kuomba Mahakama kumpa kompyuta, Mshatakiwa alipinga suala hilo na kutaka asitumie kompyuta ya Mahakama bali atumie kompyuta yake ambayo alifanyia uchunguzi tangu awali.
Upande wa Jamhuri nao uliungana na Mshtakiwa kwa kutaka Mahakama iridhie atumie kompyuta za Mahakama sauala ambalo liliendelea kupingwa vikali na Lissu.
Baada ya mvutano huo, Jaji Nduguru anayesikiliza kesi hiyo ameieleza Mahakama kuwa lazima kuwe na kifaa halisia kwa ajili ya matumizi yake hivyo ameahirisha kwa muda wa saa moja na nusu kesi hiyo kwa ajili ya shahidi kuja na kompyuta yake kujiridhisha.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.