
Kanali Michael Randrianirina ametawazwa kuwa Rais wa mpya wa Jamhuri ya Madagascar leo Ijumaa, Oktoba 17, 2025, huko Antananarivo. Tukio hili linakuja siku tatu baada ya Bunge la taifa kumuondoa Mkuu wa Nchi Andry Rajoelina na mamlaka kuchukuliwa na jeshi.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii inaashiria hatua mpya katika misukosuko ambayo imeitikisa Madagascar tangu kuanza kwa vuguvugu kubwa la maandamano ya kijamii lililoanza Septemba 25, 2025. Maanfamano haya haswa yalisababisha kuondoka nchini kwa Mkuu wa Nchi Andry Rajoelina mnamo Oktoba 12, na kufuatiwa na kutimuliwa kwake na Bunge la taifa mnamo Oktoba 14.
Leo Ijumaa, Oktoba 17 Kanali Michael Randrianirina, afisa yuleyule aliyewataka wanajeshi kukataa “kulipwa kwa kuwafyatulia risasi marafiki zetu, kaka zetu, dada zetu” waandamanaji na ambaye alitangaza mamlaka kuchukuliwa na jeshi, ameapishwa rasmi kuwa Rais wa mpya wa Jamhuri ya Madagascar. Ameapishwa mbele ya majaji wa Mahakama Kuu ya Katiba ya nchi hiyo. Ametunukiwa “Grand Cross, Daraja la Kwanza la Agizo la Kitaifa,” daraja linalopewa marais pekee.
Hii ni mara ya kwanza kwa kiapo kufanyika katika Mahakama Kuu ya Kikatiba (HCC), anaripoti mwandishi wetu maalum, Liza Fabbian. Hatu hiyo ilichukuliwa “kwa ajili ya utulivu,” kulingana na taarifa iliyotiwa saini na Kanali Michael siku mbili zilizopita. Kwa kawaida, aina hii ya sherehe hufanyika kwenye uwanja, mbele ya maelfu ya watu. Lakini kwa kkufanya uzinduzi huu katikati mwa HCC, serikali mpya katika Kisiwa hki kikubwa bila shaka inatumai kuweka uhalali wake wa kikatiba na kiishara.
Magari ya wanadiplomasia kutoka Uingereza au China, yameonekana yakiingia katika makao makuu ya Mahakama ya Kikatiba. Mabalozi wa Ufaransa, Uswisi, na Ujerumani, pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, pia wameonekana. Wanasiasa pia wamekubali mwaliko huo, akiwemo Rais wa zamani Marc Ravalomanana na Ruphin Zafisambo, aliyeteuliwa kuwa Waziri Mkuu Oktoba 6 na Andry Rajoelina.
Kanali Randrianirina alifika makao makuu ya HCC akiwa amevalia nguo za kiraia, lakini akakaa juu ya gari la kivita, akiwa ameandamana na askari wenye silaha na waliojifunika nyuso zao, kana kwamba alikuwa katika mazoezi ya kukusanyika kwake na waandamanaji na kuingia kwake katikati mwa mji mkuu wa Madagascar Jumamosi iliyopita.
Mashauriano yalifanyika katika muda wa siku tatu zilizopita na wale walioongoza maandamano ya vijana katika wiki za hivi karibuni. Hata hivyo, mashaka yanaendelea kuhusu jinsi ya kukabiliana na serikali mpya na mustakabali wa uhamasishaji. Mkutano mdogo umefanyika kwa ufupi asubuhi ya leo mbele ya HCC kuutaka utawala mpya kuendelea kusikiliza wananchi.