Kanali wa kijeshi, Michael Randrianirina, ameapishwa leo Ijumaa kuwa rais wa Madagascar katika mji mkuu, Antananarivo huku umuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) ikimteua Rais wa zamani wa Malawi Joyce Banda kuongoza ujumbe wa kutafuta ukweli nchini Madagascar kufuatia matukio ya hivi karibuni ya kisiasa na kiusalama nchini humo.

Wanajeshi wataongoza nchi ya Madagascar kwa muda wa miaka miwili na baadaye kuitisha uchaguzi mwingine.

Uteuzi wa Joyce Banda kuongoza timu ya SADC umetangazwa kwenye taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Ushirikiano wa Kisiasa, Kiulinzi na Kiusalama, Peter Mutharika ambaye pia ni rais mteule wa Malawi. Amesema: SADC inafuatilia “kwa wasiwasi mkubwa” matukio ya kisiasa na kiusalama nchini Madagascar, na kwamba SADC “imesikitishwa na ripoti za kutokea jaribio la mapinduzi ya kijeshi, ambayo yanatishia sana amani, utulivu na utaratibu wa kidemokrasia wa nchi hiyo.”

Mutharika ametangaza kuwa SADC inaonesha “mshikamano wa kina” na wananchi wa Madagaska, na amesisitizia dhamira isiyoyumba ya jumuiya hiyo ya kikanda kuisaidia Madagascar katika juhudi zake za kurejesha amani, kudumisha mfumo wa katiba na kulindwa utawala wa kidemokrasia.

Kanali Michael Randrianirina wa Madagascar katika magwanda ya kijeshi

Kwa mujibu wa taarifa ya Mutharika, Peter Banda ataongoza ujumbe wa kutafuta ukweli unaojumuisha wajumbe wenzake wa SADC wa Jopo la Wazee ili kushirikiana na serikali ya Madagascar na wadau wengine wa nchi hiyo katika juhudi za kupunguza mvutano na kuweka mazingira mazuri ya mazungumzo jumuishi. Kwa mujibu wa taarifa ya Mutharika, matokeo na mapendekezo ya ujumbe huo yanatarajiwa kuwasilishwa kwa Mwenyekiti wa SADC na baadae kwenye Mkutano wa Troika ya SADC.

Tayari SADC imetoa mwito kwa pande zote zinazohusika katika mgogoro wa hivi sasa wa madagascar “kuchagua njia ya kujizuia, amani na mazungumzo” ili kuepusha kupoteza maisha watu zaidi kutokana na machafuko hayo ambayo mwisho hakutakuwa na njia nyingine isipokuwa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *