KMC vs MBEYA CITY: Kocha wa KMC, Marcio Maximo amesema kikosi chake hakikupata muda wa kutosha wa maandalizi kabla ya kuanza msimu mpya kutokana na kuwa na majukumu ya michuano ya CECAFA Kagame Cup, lakini mapumziko ya kalenda ya FIF waliyoyapata hivi karibuni, yamewasaidia sana katika kiwanja cha mazoezi.
Maximo anasema kesho kutakuwa na burudani kwasababu timu zote mbili zinacheza mpira mzuri.
Kwa upande wa mchezaji Oscar Paul wa KMC anasema wanaitaka mechi hiyo dhidi ya Mbeya City na maandalizi yamekamilika.
Mechi ni saa 10:00 jioni LIVE #AzamSports1HD
(Imeandikwa na @allymufti_tz)
#NBCPL #NBCPremierLeague