Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, amesema kuwa kutokana na kuwepo kwa kiwango kikubwa cha uharibifu wa mazingira nchini, kinachosababisha kuvuruga ikolojia na kutishia shughuli za utalii, ni vyema suala la utunzaji wa mazingira likapewa kipaumbele katika uendelevu wake.
Dkt. Mpango ameyasema hayo mkoani Arusha, wakati wa uzinduzi wa Makumbusho ya Jiopaki ya Ngorongoro–Lengai wilayani Karatu, mkoani Arusha.
Amesema kuwa eneo hilo ni zao jipya la utalii lenye lengo la kusimulia hadithi za kale, ikiwemo mtiririko wa lava na alama za nyayo za kale, likiunganisha ikolojia na utamaduni wa eneo la Ngorongoro kama hazina yenye umuhimu wa kimataifa.
Mradi huo umegharimu takriban shilingi bilioni 32 za Kitanzania.
✍ Ramadhani Mvungi
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates