.

Chanzo cha picha, Raila/Facebook

    • Author, Abdalla Seif Dzungu
    • Nafasi, BBC Swahili
    • X,

Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya na kiongozi mkongwe wa upinzani Raila Odinga amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 80.

Akiwa mmoja wa watu mashuhuri wa kisiasa nchini humo, Odinga aliweka demokrasia ya kisasa ya Kenya katika maisha yake kwa zaidi ya miongo minne.

Licha ya kutofanikiwa kushinda urais, alisifiwa kwa kusaidia kusambaratisha utawala wa chama kimoja cha Kenya chini ya rais Daniel arap Moi mwaka wa 1992 na kupigania katiba ya mwaka wa 2010, ambayo ilileta mageuzi makubwa ya kisiasa.

Yafuatayo ni mambo matano makuu kuhusu Raila Odinga

1. ‘Handishake’ na marais wote isipokuwa Jomo Kenyatta

Alifanya handshake kwa mara ya kwanza mnamo 1997, katika hatua ya kushangaza baada ya miaka mingi ya kuwekwa kizuizini na serikali ya Moi.

Raila alikivunja chama chake cha National Development Party (NDP) ili kuungana na chama tawala cha KANU, ambapo alikabidhiwa wadhifa wa katibu mkuu wa chama hicho na wizara ya Nishati.

Mkataba huo wa maelewano (MOU) ulikuwa mbinu ya Rais Moi kuendelea kuhudumu lakini uliporomoka mwaka wa 2002 wakati Moi alipomtaja Uhuru Kenyatta kama mrithi, hali iliomfanya Raila na viongozi wengine wengi kujiondoa serikalini na kusababisha kuzaliwa kwa chama cha Liberal Democratic Party (LDP).

Mnamo 2008, alipeana mkono { Handishake} na Rais Mwai Kibaki na akapewa wadhifa wa Waziri Mkuu kufuatia ghsia za baada ya uchaguzi ambao ‘alidaiwa’ kushinda.

Mwaka 2018, alifanya handishake nyengine na Rais Uhuru Kenyatta baada ya matokeo ya uchaguzi uliopingwa na mahakama ambapo alisusia marejeleo yake yaliomfanya Uhuru kutangazwa mshindi.

Katika uchaguzi wa 2022 baada ya kushindwa na William Ruto, Raila Odinga sasa ni sehemu ya serikali pana.

Kiongozi huyo alifanya Handshake na Rais Ruto baada ya kubainika kwamba uungwaji mkono wake hasa katika maeneo ya mkoa wa kati uliompigia kura kwa wingi wakati wa uchaguzi uliopita wa 2022 ulikuwa umepungua kufuatia kuondolewa madarakani kwa kinara wa eneo hilo na aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua.

Vilevile maandamano ya Gen Z yaliopelekaa bunge kuvamiwa na vijana hao na kuchomwa yalimshinikiza Rais Ruto kumtafuta Raila Odinga kwa ushirikiano hatua iliosababisha kuundwa kwa serikali shirikishi au {Broadbased Government}

Handishake yake na Ruto ilimfanya Raila kuungwa mkono na serikali katika uchaguzi wa AU ambapo aliwasilisha ombi lake. Pia alipatiwa nafasi za mawaziri katika serikali ya Kenya kwanza.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

2. Mapinduzi ya 1982 Kenya

Saa 3 asubuhi Jumapili, 1 Agosti 1982, kikundi cha wanajeshi kutoka Jeshi la Wanahewa la Kenya wakiongozwa na Senior Private Hezekiah Ochuka walijaribu kupindua serikali ya rais wa wakati huo Daniel Arap Moi.

Baada ya jaribio lililofeli la kupindua serikali yake , Rais Moi alipanga upya usalama wa serikali yake na kuwaweka baadhi ya wandani wake na kisha akahakikisha sheria inapitishwa bungeni ambayo ilimpa mamlaka ya dharura huku akiweka utawala wa mkoa chini ya ofisi ya rais.

Wakati huo Raila Odinga alikamatwa na kushtakiwa kwa uhaini baada ya kushutumiwa kuwa miongoni mwa waanzilishi wa mapinduzi ya hayo.

Aliachiliwa miaka sita baadaye mnamo Februari 1988 lakini akawekwa kizuizini tena mnamo Agosti mwaka huo huo na kuachiliwa mnamo Juni 1989.

3. Uchaguzi wa 2007 uliokumbwa na ghasia

Tarehe 27 mwezi Desemba 2007 Uchaguzi mkuu ulifanyika nchini Kenya.

Wapiga kura walimchagua Rais, na wajumbe wa Bunge la Kitaifa. Uchaguzi huo pia uliambatana na uchaguzi wa mitaa Kenya.

Mwai Kibaki, aliyegombea kwa tiketi ya chama cha Party of National Unity (PNU), alimshinda Raila Odinga, kiongozi wa Orange Democratic Movement (ODM) na Kalonzo Musyoka wa Orange Democratic Movement–Kenya.

Uchaguzi huo ulikuwa na uhasama mkubwa wa kikabila, ambapo Kibaki aliungwa mkono na watu wa kabila lake la Wakikuyu naye Raila Odinga ambaye ni mtu kutoka kabila la Wajaluo akifanikiwa kuunda Muungano na viongozi kutoka makabila ya Magharibi , Bonde la Ufa, Pwani na kaskazini mwa Kenya.

Hatahivyo Kibaki ndiye aliyetangazwa mshindi akiwa na asilimia 46 ya kura hizo na kuapishwa kuwa rais .

Raila Odinga alipinga matokeo hayo akidai kuwa yeye ndiye aliyeshinda uchaguzi huo. Hatua hiyo ilisababisha ghasia zilizosababisha mauaji ya Wakenya wengi huku zaidi ya watu lakini sita wakiachwa bila makao.

Hali hiyo lilihitimishwa na Sheria ya Makubaliano ya Kitaifa na Maridhiano, ambayo ilipelekea Odinga kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu.

Katika uchaguzi wa Bunge la Kitaifa, ODM ilishinda viti 99 kati ya 208, huku PNU ikimaliza ya pili kwa viti 43.

Kulingana na Wikipedia hatahivyo kuna makubaliano katika jumuiya ya kimataifa kwamba uchaguzi huo wa urais ulichakachuliwa angalau kwa kiasi.

Mnamo Julai 2008, kura ya maoni iliyoidhinishwa na Marekani ilitolewa, na kupendekeza kuwa Odinga alitabiriwa kushinda urais kwa tofauti ya asilimia 6, 46% hadi 40%, nje ya asilimia 1.3 ya makosa ya kura hiyo.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

4. ‘Alijiapisha’ kama rais wa raia Kenya

Mnamo tarehe 30 mwezi Januari 2018

Raila Odinga alikula kiapo kisicho rasmi cha “kuapishwa” kama rais wa raia licha ya vitisho kutoka kwa serikali kwamba angeshtakiwa na kosa la Uhaini wakati wa serikali ya Uhuru Kenyatta.

Odinga alikula kiapo chake akishangiliwa na maelfu ya wafuasi waliokuwa wamekusanyika katika bustani ya Uhuru Park Nairobi.

Wakati huo usalama katika mji mkuu wa Kenya ulikuwa umeimarishwa kabla ya sherehe hiyo huku mamlaka ikifunga vituo huru vya televisheni.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

5. Raila alifahamu kuhusu kifo cha mama yake baada ya miezi miwili

Waziri Mkuu huyo wa zamani wa Kenya alifahamu kuhusu kifo cha mamake baada ya miezi miwili kupita

Ni ukweli unaojulikana sana kutokana na wasifu wa Raila Odinga kwamba alifungwa gerezani mwaka wa 1982.

Alishutumiwa kuhusika na jaribio la mapinduzi mwaka huo huo. Mamake Raila , Mary Juma Odinga, aliaga dunia miaka miwili baadaye mwaka wa 1984.

Raila Odinga aliyefungwa hakujulishwa kuhusu ukweli huu na akapata habari hiyo ya kusikitisha miezi miwili tu baadaye.

Aliachiliwa kutoka gerezani mnamo Februari 6, 1988.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *