BAADA ya mapumziko ya kupisha kalenda ya Fifa kumalizika wiki hii, kipute cha Ligi Kuu Bara kinaendelea jana ikishuhudiwa mechi mbili kati ya Pamba Jiji iliyoikaribisha Mashujaa mjini Mwanza, huku Fountain Gate ikiwa ikiwakaribisha Dodoma Jiji, lakini leo pia kuna kipute cha aina yake.

Leo, KMC inaikaribisha Mbeya City, ukiwa ni mchezo wa kwanza kukutana kwa timu hizo tangu msimu huu uanze.

Ikumbukwe kuwa Mbeya City siyo wageni wa michuano hii, lakini inakwenda kucheza kwa mara ya kwanza katika Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam kwani msimu huu ndio imerejea Ligi Kuu Bara baada ya kushuka miaka miwili iliyopita.   

MBE 03

Mpaka sasa timu zote mbili zimecheza mechi tatu ambapo KMC inashika nafasi ya 12 na Mbeya City ikiwa namba nane.

KMC kwa rekodi iko chini ikiwa na pointi tatu ilhali Mbeya City ikiizidi alama moja, imefungwa mechi moja, sare na suluhu moja moja. Nayo KMC imecheza mechi tatu ikishinda moja na kupoteza mbili. 

MBE 04

Mbeya City inaonekana kuwa na nguvu hasa ugenini, ingawa wakati mwingine hujikuta ikipoteza nafasi za kufunga. Pia  imekuwa na mechi nyingi za sare au kufungwa kwa tofauti ndogo dhidi ya timu inazoshindana nazo. Hii inaonyesha kuwa ina uwezo wa kuhimili vishindo vya wapinzani na kuwatuliza kwa suluhu au sare.

MBE 01

UTAMU UKO HAPA 

KMC ina rekodi nzuri dhidi ya Mbeya City katika mechi za hivi karibuni hasa pale inapocheza nyumbani ikiwa na uwezo wa kushambulia vizuri na pia kulinda lango lake, kwani katika mechi tatu, mbili imechezea nyumbani ikifanikiwa kuichakaza Dodoma Jiji bao 1-0, huku ikiruhusu bao moja dhidi ya Singida Black Stars.

Mbeya City imekuwa haitabiriki ugenini kwani imepoteza mara moja dhidi ya Azam 2-0 na kuifunga Fountain Gate kwake 0-1.

MBE 02

WASIKE MAKOCHA

Akizungumzia mchezo huo, kocha wa KMC, Marcio Maximo alisema mapumziko ya kalenda ya Fifa yamewasaidia katika uwanja wa mazoezi kuhakikisha kwamba wanatengeneza ubora ili kuweza kushindana katika mashindano yanayowakabili.

“Leo kutakuwa na burudani kwa sababu timu zote mbili zinacheza mpira mzuri, hivyo tunategemea kufanya vyema kwa sababu tayari tumeshughulikia makosa ya mechi zilizopita,” alisema Maximo.

Naye Oscar Paul, mchezaji wa timu hiyo alisema: “Tunaitaka mechi dhidi ya Mbeya City na maandalizi yamekamilika, kwani tayari tumeshawasoma wapinzani.” KMC inaikaribisha Mbeya City ikiwa ni mechi ya nne kwa kila moja na mchezo huo utaanza  10:00 Jioni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *