Mjane Ida Odinga amewaomba Wakenya na mataifa jirani ya Afrika Mashariki, kumuomboleza Hayati Raila Amolo Odinga kwa amani wakati huu, familia na wafuasi wa kiongozi huyo wa zamani wa upinzani na Chama cha ODM wakiwa kwenye simanzi ya kuondokewa na mpendwa wao.
Ida ametoa ombi hilo leo kwenye mazishi ya kitaifa aliyofanyiwa Odinga, ambaye ni waziri mkuu wa zamani wa Kenya, katika uwanja wa Nyayo uliopo jijini Nairobi, ambapo viongozi kutoka mataifa mbalimbali wamehudhuria, akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.
Hayati Odinga alifariki Jumatano Oktoba 15, 2025 nchini India; na mwili wake utazikwa Jumapili hii nyumbani kwake Bondo, baada ya kufanyiwa ibada ya mazishi kesho kwenye uwanja wa Moi Kisumu.
✍ @abuuyusuftz
#RIPRailaOdinga #RIPOdinga #Baba