Mkurugenzi wa Tathmini na Majaribio kutoka Taasisi ya Uthibitishaji wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Matengia Swai, amewataka wakulima…Mkurugenzi wa Tathmini na Majaribio kutoka Taasisi ya Uthibitishaji wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Matengia Swai, amewataka wakulima…

Mkurugenzi wa Tathmini na Majaribio kutoka Taasisi ya Uthibitishaji wa Mbegu Tanzania (TOSCI), Matengia Swai, amewataka wakulima kote nchini kuhakikisha wanajisajili kwenye mfumo wa ruzuku ili waweze kunufaika na upatikanaji wa mbegu bora kwa gharama nafuu.

Swai ametoa wito huo wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Chakula Duniani yaliyofanyika kitaifa jijini Tanga, ambapo wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo walikusanyika kujadili changamoto na fursa zilizopo katika sekta hiyo muhimu.

Ameongeza kuwa usambazaji wa mbegu zisizothibitishwa umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzalishaji na ubora wa mazao nchini, hivyo ni muhimu kwa wakulima kutumia mbegu bora zilizopitia tathmini ya kitaalamu kutoka TOSCI.

#startvupdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *