PACOME MAZOEZINI KUIWINDA SILVER STRIKERS
Kiungo wa Yanga SC, Pacome Zouzoua leo amefanya mazoezi mepesi kwenye uwanja wa Taifa wa Bingu Jijini Lilongwe kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji wao, Silver Strikers.
Pacome aliwasili jana mchana na akitokea nchini kwao, Ivory Coast ambako aliisaidia kufuzu Kombe la Dunia 2026 baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kenya.
Baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kamuzu na kupokewa na Mratibu wa Timu, Hafidh Saleh – Pacome alikwenda moja kwa moja kwenye Dimba la Taifa la Bingu kufanya mazoezi na wenzake ambao waliwasili jana asubuhi wakitokea Dar es Salaam.
Mechi ni kesho saa 10 jioni LIVE #AzamSports1HD
#CAFCL #YangaSC #YangaMalawi #Pacome
(Feed generated with FetchRSS)