Mgombea Udiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Kata ya Chanika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga, Habibu Mbota maarufu kama “Mojakwamoja”, amefanya ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara wa masokoni eneo la Mkwajuni, maarufu kama Walumba, ambapo aliwasilisha dhamira yake ya kuboresha ustawi wao endapo atachaguliwa.
Katika mkutano huo, Mbota alieleza jitihada kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na wasaidizi wake katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.
Akiwa mbele ya wafanyabiashara hao, Mbota aliahidi kuwakatia bima za afya bila malipo wabeba mizigo wote wa eneo hilo, ili kuhakikisha wanapata huduma bora za afya bila vikwazo. Alieleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya mkakati wake wa kuhakikisha kuwa kundi hilo linalofanya kazi ngumu linaepuka madhila ya gharama za matibabu.
Aidha, aliahidi kuwa atakuwa mstari wa mbele katika kushughulikia kila kero inayowakabili wafanyabiashara hao.
#StarTvUpdates
(Feed generated with FetchRSS)