Rais mstaafu wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais wa sasa Dkt. Philip Mpango wamewasili jijini Nairobi, Kenya, kwa ajili ya kushiriki ibada ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Amollo Odinga.

Ibada hiyo imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Nyayo, huku shughuli za kuaga mwili zikiendelea leo katika Majengo ya Bunge, ambako Raila aliwahi kuhudumu kama Mbunge wa Kibra kwa takribani miaka 20.

Rais wa Kenya William Ruto ameongoza wabunge na viongozi mbalimbali kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi huyo mashuhuri ambaye aliheshimika ndani na nje ya Kenya kwa mchango wake mkubwa katika siasa, demokrasia na maendeleo ya Afrika Mashariki.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *