
Waasi wa Houthi wametangaza siku ya Alhamisi, Oktoba 16, kifo cha kiongozi wao wa kijeshi, Jenerali Mohammed al-Ghamari. Waasi wa Houthi hawakueleza mazingira ya kifo chake, lakini Waziri wa Ulinzi wa Israel amesema kuwa Mohammed al-Ghamari alifariki kutokana na majeraha aliyoyapata katika shambulizi la Israel mwezi uliopita wa Agosti.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Shambulio ambalo Mohammed al-Ghamari aliuawa pia liliua Waziri Mkuu wa Houthi na maafisa wengine kumi na wawili. Tangu kuanza kwa operesheni ya Israel huko Gaza, waasi wa Houthi wamedai kuwaunga mkono Wapalestina na wamekuwa wakifanya mashambulizi katika ardhi ya Israel, mara nyingi wakizuiwa. Jeshi la anga la Israel lilishambulia kwa mabomu katika maeneo kadhaa ya Wahouthi nchini Yemen.
Mohammed al-Ghamari alikuwa mmoja wa washirika wa karibu wa kiongozi wa Houthi Abdul-Malik al-Houthi na mmoja wa wanajeshi wake wenye uzoefu mkubwa. Alikuwa mkuu wa shirika la operesheni za hivi karibuni dhidi ya Israel.
Taarifa ya Houthi iliyotolewa leo ikitangaza kifo chake haiitaji moja kwa moja Israel kuhusika. Lakini kundi la waasi la Yemen hata hivyo linasisitiza kwamba “mapambano na adui wa Israel hayajaisha” na kwamba “itapata adhabu ya kuzuia kwa uhalifu liliofanya.”
Baada ya kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas wiki iliyopita, Wahouthi walithibitisha kuwa wako katika hali ya tahadhari na watafuatilia kwa karibu utekelezaji wake kabla ya kufikiria kusimamisha shughuli zao.